Sitosahau Mganga wa Kienyeji Alichonifanyia Mpaka Nikampa..

Nilikuwa na mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati yaani nilikuwa nipo tayari hata anioe. Lakini mwenzangu hakuwa na upendo kama wangu, alikuwa ananisumbua sana na ana maudhi mengi japokuwa niliyavumilia sababu nilikuwa nampenda sana.

Mara kwa Mara nilikuwa nikilalamika kwa yale anayonifanyia ili abadilike lakini wapi. Jambo hili lilikuwa linaniumiza sana hadi kuna siku aliniambia kuna mwanamke anampenda sana. Yaani ana mpenzi mwngine kwa hiyo mapenzi yake yameamia kwa huyo mpenzi mpya.

Kila siku nilikuwa nawaza itakuwaje labda atabadilika, ila kuna wazo likanijia niende kwa mganga nikamfanyie dawa anipende na ikiwezekana anioe kabisa. Tangu nizaliwe sikuwahi kwenda kwa mganga so waganga nilikuwa  siwajui kabisa.

Nikawaza mbona njiani huwa nakutana na mabango ya mganga kutoka Nigeria, Rukwa, Bagamoyo nk? Nikasema nikiona bango nitachukua namba nipige nielekezwe niende.

Ni kweli niliona bango nikachukua namba nikapiga tukaongea. Akanielekeza ni maeneo ya Tandika lakini ndani ndani. Nikajianda nikaenda, hadi kufika alipo huyo mganga pikipiki inahusika.

Nikafika hadi mtaan kwake kuna dada akaja kunichukua barabarani nikaongoza naye hadi alipo huyo mganga(nyumbani kwake). Nilipoingia ndani tu kabla ya kuingia chumba cha mganga huyo dada akaniambia “kabla ya kuingia kumuona babu unapaswa utoe 5000 uweke hapo ndio masharti”. Nikatoa, akaniambia subiri babu yupo na mteja anamhudumia.

Nikasubiri pale kama dakika kadhaa akatoka kweli mtu nikaingia. Kweli chumba kilikuwa na mazingira yote ya kiganga kama ofisi za waganga zinavyokuwa. Jamani hiko chumba cha babu kina giza japo ilikuwa mchana akaniambia niwashe mshumaa(kulikuwepo na mshumaa). Baada ya kuwasha kukapatikana mwanga hafifu.

Akaanza kuniuliza “nini shida yako?” Nikamuelezea kama nilivyoandika mwanzo akasema “aah kwahiyo unataka atulie na wewe akupende?” Nikajibu ndio, akasema ok, kwanza ntakupa dawa ya kutengeneza uchi wako akiingia tu asikusahau, ila hiyo dawa lazima nipate na shahawa zake huyo mwanaume tuchanganye ujipake wewe kwenye uchi wako.

Niliguna nikamwambia hiyo ni ngumu mimi kupata shahawa zake hata nikienda kufanya nae ntazichukuaje asione? Akasema usijali mimi nitakusaidia nitapaka hii dawa dudu langu halafu nitakupaka kutumia dudu langu kwenye uchi wako kwa juu juu ntaingiza kichwa tu.

Nikaguna nikawa mtu mwenye wasiwasi nikawaza huyu anataka kunifanya vibaya nini? Mganga akasema usihofu hakuna baya litakalo tokea ni hvyo tu nataka nikusaidie. Ungeweza nilivyokuambia mwanzo ungechukua shahawa za bwana ako ungechanganya na dawa ungefanya mwenyewe lakini umesema huwezi.

Nikatulia kweli akapaka dawa kwenye kichwa cha uume yake akaniambia nivue chupi ntanue miguu huku nikiwa nimekaa na yeye amekaa. Nikafanya hvyo sikuvua nguo zote sababu nilivaa gauni. Kwahiyo nilifanya kulifunga tumboni, akanisogelea akaniambia tanua vizuri naingiza kichwa tu kwa juu juu kweli nikafanya hivyo.

Mara nikaona anapitiliza siyo kichwa tena imeingia na kiwiliwili yaani nilikasirika ghafla nikamsukumiza hata yeye aliona nimepaniki. Akasema tayari dawa nishaingiza kazi iliyobaki kwenda kununua dawa nyingne na njiwa atawatuma hadi ninapokaa nitawaona juu wakipita njiwa wawili weupe mida ya saa 10 kamili jioni.

Akaniomba pesa ya dawa afanye kazi, nikamuuliza bei gani. Akajibu 15,000 tu,nikamwambia sina nina 5000 tu maana nilikuja na 10,000/- na kuna binti kaichukua nyumbani kwako kama masharti kabla ya kuonana na wewe.

Akasema sawa lakini kama alisitasita. Nilikuwa na 7000 imebaki hivyo 5000 nilimpa na 2000 nikabaki nayo nifanye nauli ya kunirudisha home. Nikampa nikaondoka zangu, nikafika nyumbani nikakaa hadi hiyo saa 10 kamili sikuona njiwa wala kitu gani na mambo hayakubadilika chochote.

Nikawa nimeshaliwa na mganga bila kupenda

Joyce

Previous Entries SHIRIKA LA WWF LAFANYA ZIARA KUFUATILIA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MRADI WA SECAD WILAYANI NAMTUMBO Next Entries HABARI KUTOKA UMOJA WA MATAIFA