Statement ya Simba SC Kuhusu Kauli ya Kabwili wa Yanga SC

Ni siku moja imepita toka golikipa wa Yanga SC Ramadhani Kabwili kuituhumu club ya Simba SC kuwa iliwahi kumuahidi hongo ya gari Toyota IST, endapo angekubali kujipatisha kadi ya tatu ya njano katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, ukiwa ni mchezo mmoja kabla ya game ya watani wa jadi.

Kama Kabwili angefanya hivyo kwa madai yake anasema kwa kuwa angekosa mchezo unaofuata kikanuni, kiongozi huyo wa Simba SC aliyemtaka kufanya hivyo aliamini kukosekana kwake kungelazimika Yanga kumchezesha Kindoki ambaye kimsingi kwa wakati huo alikuwa hafanyi vizuri katika soka.

Leo Simba SC imetoa msimamo wake na kueleza kukerwa na kauli ya Kabwili ila haijachukua hatua yoyote kwakuwa, mamlaka husika (TFF) imechukua hatua za haraka kuhusiana na hilo, hivyo kama Simba SC imeliachia mamlaka husika kuhusiana na hilo

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Previous Entries Samatta Atinga Fainali, Aston Villa yaichapa Leicester City Next Entries MRADI WA KUJENGEA UWEZO WATAALAM NA WAKULIMA KATIKA KILIMO CHA AUMWAGILIAJI WAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA. DODOMA