https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

 
Monday September 20 2021
Tamisemi pc
Dodoma. Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) nchini Tanzania imesema inashughulikia malalamiko ya mawili ya rushwa katika zoezi la upandishaji wa madaraja kwa walimu lililofanyika hivi karibuni.
Hayo yamesema leo Jumatatu Septemba 20, 2021 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweri wakati akifungua mafunzo kwa makatibu wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC).
Amesema pamoja na mafanikio makubwa iliyoipata tume hiyo bado kuna malalamiko ya rushwa hasa katika upandishaji wa madaraja.
“Tuna malalamiko ya baadhi ya watumishi kuomba rushwa na hili lazima tuliseme na kwasasa hivi tuna kesi mbili tunashughulikia za watumishi kwasababu bado kesi hizi zinaendelea siwezi kusema kwasababu gani?” amesema.