UJERUMANI YAZINDUKA NA KUICHAPA URENO YA RONALDO 4-2 MUNICH

UJERUMANI imezinduka na kuichapa Ureno 4-2 katika mchezo wa Kundi F Euro 2020 leo Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Rúben Dias dakika 35, Raphael Guerreiro dakika ya 39 wote wakijifunga, Kai Havertz dakika ya 51 na Robin Gosens dakika ya 60, wakati ya Ureno yamefungwa na Cristiano Ronaldo dakika 15 na Diogo Jota dakika ya 67.
Ujerumani sasa ina pointi tatu sawa na Ureno, wakiwa nyuma ya Ufaransa inayoongoza kwa pointi zake nne na mbele ya Hungary yenye pointi moja baada ya mechi mbili mbili za mwanzo.

Previous Entries WAZIRI MKUU AKOSHWA NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA AFRICAB Next Entries DIWANI VITI MAALUM LIDYA MGAYA AUNGA MKONO UJENZI WA S/M KALABAKA