Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Milinde Mahona akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Gofu kwa Makapuni ya Kibiashara ya Corperate Masters 2021 yenye lengo la kujenga mahusiano na ushirikiano wa kibishara, katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Kapteni wa Gofu, Fred Laizer. Kushoto ni Mwenyekiti wa mashindano hayo, Kelly Kariuki, Kulia ni Mchezaji wa Gofu Klabu ya Lugalo, Nathan Mpangala, Kapteni wa Gofu, Fred Laizer na Mdhamini wa mashindano kutoka Benki ya CRDB, Gibson Mlaseko.
Mwenyekiti wa mashindano ya Gofu kwa Makapuni ya Kibiashara ya Corperate Masters 2021, Kelly Kariuki, akizugumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mashindano hayo yenye lengo la kujenga mahusiano na ushirikiano wa kibishara uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Kapteni wa Gofu, Fred Laizer.

AFISA Maendeleo wa Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa, (BMT) Milinde Mahona amesema michezo ni sehemu ambayo watu wanaweza kukutana na kupata marafiki wapya ambao wanaweza kufanya baishara, kwa hiyo ameziasa Kampuni mbali mbali zijitokeze kufadhili michezo.

Mahona amezungumza hayo mwishoni mwa wiki, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Golf kwa makampuni ya kibiashara yanayojulikana kama Corporate Masters 2021. Yaliyofanyika katika viwanja vya Golf vya Gymkana jijini Dar es Salaam.

“Michezo ni fursa kubwa kwa wadau kuonesha namna wanavyoweza kuwa pamoja, nawapongeza wote waliojitokeza na waliyojiunga na mchezo wa golf kutoka kampuni mbali mbali, na ninaahidi kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika michezo,” amesema Mahona.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Corporate Masters Golf Competition, Kelly Kairuki amesema mashindano ya Golf kwa Makammpuni ya Kibiashara yanayojulikana kama Corporate Masters Golf ametoa wito kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa golf kutoka makampuni na mashirika mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki kilele cha Corporate Masters golf competition 2021, kitakachofanyika Agosti 7 2021 katika viwanja hivyo.

Amesema, mashindano hayo yanatoa fursa kwa wafanyakazi wa makampuni ya kibiashara na wafanyabiashara kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu biashara na uchumi huku wakicheza Golf.

“Lengo kubwa la mashindano haya ni kuwaleta pamoja mameneja na wafabyabiashara tofauti kukutana na kwamba mbali na kucheza pia wataweza kubadirishana mawazo kutangaza biashara zao na kuwezeshana kama wafanyabiashara kwa kuchangiana mawazo ambayo yataboresha sekta nzima ya bu biashara na michezo na kukuza uchumi wa nchi yetu’. Amesema Kelly.

“Tunaishukuru club ya Gymkana kwa kutuwezesha kuwa hapa, lakini pia naishikuru serikali kwa kutuwezesha kuwa hapa na kutupa ushirikiano mkubwa. Aidha, tunawashukuru wadhamini wetu mbali mbali wakiojitokeza kufanikisha mashindano haya.” Alisema Kairuki

Naye, Mdhamini Mkuu wa mashindano hayo, Gibson Mlaseko ambaye ni Meneja Mwandamizi wa huduma ya Primier na Benki kutoka CRDB ameema mashindano hayo ni mazuri kwa sababu yanawakutanisha wafanyabiashara pamoja.

“Sisi kama Benki ya CRDB tunatoa ushirikiano katika michezo, lakini tumeona katika eneo hili la Golf ni eneo nzuri linaleta wadau kutoka maeneo mbali mbali. Hivyo tumeona hii ni fursa adhimu ya kuweza kukutanisha watu kwa ajili ya kuweza kuboresha biashara zao,” amesema

Akizungumizia, maandalizi ya mashindano hayo, alisema yameandaliwa vizuri, ambapo wanategemea katika kilele chake kitakuwa bora zaidi na ni fursa kwa wao kukutana na wa wadau wa sekta mbali mbali za uchumi na kuangalia namna watavyoweza kushirikiana na kuboresha thamani katika maeneo yao.

Mdhamini wa mashindano ya Golf kwa makampuni ya kibiashara ‘Corporate Masters Golf 2021’ kutoka CRDB, Gibson Mlaseko akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Milinde Mahona na kushoto ni kapteni wa Gofunch uwanja wa Gymkana Fred Laizer

Matukio mbalimbali ya uzinduzi wa Corporate Masters 2021 viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaa