Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kumuombea Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, ili aweze kufanikiwa katika klabu yake mpya ya Aston Villa ambayo amesaini mkataba wa miaka 4 na nusu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mwakyembe  baada ya mtanzania huyo kudaka saini ya timu ya Aston Villa

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Mwakyembe amesema kuwa “hakika kama Serikali tumefurahi kama walivyofurahi Watanzania wote, tunampongeza sana Samatta kwa juhudi zake najua hakubahatisha, ila kwa nidhamu ya hali ya juu, na hiki ndiyo kinawakwamisha vijana wengi wa Kitanzania mtu akikupa safari mbili unajiona umemaliza.” Waziri Mwakyembe