Msanii Maarufu wa filamu za Kibongo , Wema Sepetu,  amempongeza Diamond Platnumz kwa video yake mpya ya ‘Iyena’ aliyomshirikisha Rayvanny.

Katika maudhui ya video hiyo, Diamond amecheza na mzazi mwenziye, Zarina Hassan (Zari The Boss lady),  kama wamefunga ndoa, Wema amemtaka msanii huyo kufanya kweli kama filamu hiyo inavyoonyesha.

“New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri,” ameandika Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram.”

Kabla ya Diamond na Zari kuwa na mahusiano yaliyowaletea watoto wawili na baadaye kutengana, mwanamuziki huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema. 
Hata hivyo, Siku ya Wapendanao (Valentine Day) mwaka huu,  Zari alitangaza kuvunja kwa mahusiano yake na mwimbaji huyo akidai alikuwa na mtandao mkubwa wa wapenzi wengine.