YANGA IS BACK- KOCHA NASREDDINE

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

“YANGA IS BACK”, Ni maneno ya Kocha Mkuu wa Yanga  Nasreddine Al Nabi  baada ya kuangalia kiwango cha wachezaji wake na kuondoka na alama tatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ilifaniiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Simba katika mchezo uliochezwa jana kwene dinmba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kocha  Nasreddine  amesema anafurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika dakika zote 90 na kufanikiwa kupata ushindi huo kutoka kwa wapinzani wake Simba,

Amesema, mchezo ulikua mzuri sana na Simba ni timu nzuri waliingia uwanjani wakiwa wamejipanga kuhakikisha hawaruhusu kufungwa na hilo limefanikiwa baada ya wachezaji wake kuonesha nidhamu kubwa sana.

“Simba naijua ni timu nzuri, na tuliingia kwa tahadari kuhakikisha haturuhusu Simba kuutawala mchezo huo na wachezaji wangu walifuata maelekezo, nimefurahi sana kupata ushindi huu,”amesema  Nasreddine

Ameeleza, ushindi wa jana dhidi ya Simba ni ishara kuwa sasa timu yake imeanza kurejea katika kiwango chake na ligi na palipo na mapungufu atafanyika kazi.

 Nasreddine  ameongezea na kusema kwa sasa wanajiandaa na michezo miwili iliyosalia wakiwa na alama 70 nyuma ya Simba walio na alama 73 wakisalia na michezo minne.

 

Previous Entries DKT. BUDEBA ATOA PONGEZI KWA WIZARA YA MADINI NA TAASISI ZAKE Next Entries UJUMBE WA KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO BAADA YA KUWASILI VISIWANI ZANZIBAR, SHAKA 'APIGILIA MSUMARI'