YANGA imetwaa taji la Ngao ya Jamii mbele ya watani zao wa jadi Simba katika mchezo uliokuwa na mvuto mkubwa.


Uwanja wa Mkapa mashabiki waliojitokeza kiasi chake na haikuwa nyomi ya kutisha zaidi ya mashabiki Yanga angalau walijitokeza kwa wingi.


Bao la ushindi limepachikwa na Fiston Mayele kwa shuti kali ambalo lilimzidi ujanja Aishi Manula kipa namba moja wa Simba.


Kiungo mkata umeme Taddeo Lwanga alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5