Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MABINGWA wa Kihistoria katika Soka la Tanzania, Young Africans SC wametwaa taji la Ngao ya Jamii 2021 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Bao pekee la Yanga SC lilifungwa na Mshambuliaji, Fiston Mayele dakika 11, baada ya kupokea asisti safi ya Winga, Farid Mussa Maliki aliyeichambua ngome ya Simba SC na kufanya mchezo huo kuisha ndani ya dakika 90 pekee.

 Katika kipute hicho Yanga SC walionekana bora zaidi katika eneo la Kiungo cha ukabaji kilichokuwa chini ya Yannick Bangala na Khalid Aucho wakiwalinda Mabeki wa kati, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5


Yanga SC imeanza msimu vyema msimu huu wa mashindano wa 2021-2022 baada ya ushindi huo ambapo Septemba 29, 2021 watafungua Pazia la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati Simba SC wakifungua Ligi hiyo na Biashara United katika dimba la Karume mjini Musoma, Septemba 28, 2021.