Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kikao cha Umoja wa Matawi Yanga umeibuka na kusema hawatakuwa tayari kusimamiwa uchaguzi wao na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tawi la Yanga Kariakoo, Kaisi Edwin, ameeleza kuwa wao kama wanachama wapo tayari kufanya kila kitu wao.

Edwin amefunguka akiwa katika munkari ya hasira akieleza wameamua kufanya hivyo kwa kuwa wana uwezo wa kujisimamia wenyewe na si kuongoza na mtu mwingine yoyote.

Aidha, Edwin ametangaza vita na wanachama Yanga ambao wataenda TFF kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea uchaguzi kwani hawatatambulika ndani ya klabu na hawataweza kuingoza Yanga.