Reposted from @zamaradimketema Kila siku wanaume wamekuwa labelled kama watu wasiofaa, washenzi na wasio na huruma kiasi hata jamii na msichana mdogo anaekuwa anaanza kuwa na Perception kuwa Wanaume Sio watu, na hiyo inaenda hadi inaathiri kwa namna moja ama nyingine mahusiano mengi maana hata anapopata alie BORA anaendelea kuishi kwa machale kiasi badala ya kujenga anaharibu, na hii inatokea sana sababu hata wanapotokea wazuri hatuwaappreciate, tunanyamanza, tunaona ni kama Dhambi kutoka mbele na kusema I am Happy, unawaza watu watanionaje tukiachana, unashindwa Kuenjoy moment kwa kuogopa kesho ambayo huifahamu, Guys MAISHA NI LEO!! Have Fun unapopata nafasi, MUNGU hajakupa Baraka uliyonayo ili ukae kwa wasiwasi, Toa maradhi ya wasiwasi ISHI!! Unajiskia kumsifia mtu wako msifie, mahaba yamekuzidi unataka kuita Press ITA!! Its your Life na una haki ya kuishi vile upendavyo bila kuvunja sheria za nchi, mambo ya kujibanabana kesho kachoropoka unakosa hata kumbukumbu nzuri utajilaumu 🤣 RIZIKI ANATOA MUNGU!! Relax!! Kama alivyoletwa bila kutumia nguvu yako basi kama ni wa kuondoka haitategemea juhudi zako za kujibana, Enjoy Life, kama walivyo wanawake wabaya na wazuri na wanaume ni hivyohivyo, Tusitangaze tu habari mbaya hata nzuri zinapotokea tusizikalie kimya

Leo acha nichukue nafasi kukuappreciate mbele za watu, WEWE NI MWANAUME NA NUSU, Mwanaume uliesimama kwenye majukumu yako na unajua mke anataka nini, natembea kifuambele unanipenda na kila changu, Hakuna mwanamke asiependa kukaa kunyoosha miguu, ila ni maisha tu, mimi umenipa hiyo nafasi, ASANTE!! Na sio kwamba sijui kutafuta, Najua kutafuta kwelikweli na ALHAMDULILLAH naipata ambayo hata kama usingekuwepo bado ningeishi maisha ya KUTAZAMWA lakini wala huna macho nayo 😆’ Bado wewe ni MWANAUME ndani ya nyumba!! Nitake nini tena, nikisubiri kutoa sifa zako mbaya tu huku mazuri yako sikuwahi kuyasema nitakuwa kama viberenge, Baby You are a MAN!! Hata itokee chochote leo haitabadilisha kuwa wewe ni mwanaume, nimegundua wanaume wa aina yako ni wachache kiasi hata anapotokea ukiongea bado watu wanakuona muongo 😀, Naachaje kukuthamini, ASANTE MUME WANGU.
NB: Haya ni ya LEO, Ya Kesho Sio shida zangu MUNGU alienipa wewe atajua anasort vipi 😆